Katibu mkuu wa ccm, emmanuel nchimbi amewataka wananchi kuwa makini wakati wa kupiga kura wakatae kuchagua viongozi wa kupandikizwa

Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi amewataka Wananchi kuwa makini wakati wa kupiga kura katika Chaguzi zijazo na wakatae kuchagua Viongozi wa kupandikizwa na Viongozi wa mfukoni.

Akiongea wakati wa ziara yake Mkoani Rukwa, Nchimbi amesema “Tutakapofika wakati wa Uchaguzi tunaanza Chaguzi za Serikali za Mitaa tunateua Makada miongoni mwetu kutuwakilisha kwenye Vyombo vya Dola, tuchague kwa umakini sana, kataeni Viongozi wa kupandikizwa, kataeni Viongozi mnaoletewa mfukoni kwamba huyu awe Kiongozi wenu”

“Nyinyi mnaishi na mnaishi na Watu kwenye maeneo yenu mnawajua, chagueni Watu kwa sifa zao sio kwa sifa za Walezi wao, Mtu ahukumiwe kwa sifa zake sio sifa za Rafiki zake, tukishaenda kwenye Uchaguzi Watu wote lazima wajue kuna mmoja atashinda na mwingine atashindwa , tukimaliza Uchaguzi tukubali matokeo tuunganishe Timu tuwe Timu moja”

“Makundi ya Uchaguzi yanatakiwa yaishe mara baada ya matokeo kutangazwa, wanaotusumbua katika Uongozi wa Chama ni wale ambao akili zao zinawaza Ubwana mkubwa”

Share: