Kampeni rasmi zimeanza nchini rwanda huku taifa hilo la afrika mashariki likijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa urais na ubunge

Kampeni rasmi zimeanza nchini Rwanda Jumamosi hii, huku taifa hilo la Afrika mashariki likijiandaa kwa uchaguzi mkuu (wa Urais na Ubunge).

Tarehe 15 Julai, wapiga kura watawachagua viongozi wao huku wagombea watatu wakigombea kiti cha Urais, akiwemo rais wa Paul Kagame, Frank Habineza, and Phillipe Mpayimana. Watu milioni tano wamesajiliwa kupiga kura.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Rwanda wagombea mia tano wameidhinishwa kupigania viti themanini vya ubunge.

Katika wiki ttau zijazo, wanasiasa hao watazuru maeneo mbali mbali nchini humo kuuza sera zao kutafuta uungwaji mkono.

Rais Kagame- ambaye amekuwa mamlakani kwa miongo miwili – anafanya kampeni kuwania kiti hicho kwa awamu ya nne. Amepata pongezi kwa kuleta amani nchini humo japo anakashifiwa kwa madai ya kuzima sauti za upinzani, madai ambayo amekana.

Share: