Kamati Ya Siasa Ya Ccm Mkoa Yaridhishwa Na Utekelezaji Wa Miradi Kinondoni

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa Dar es salaam chini ya mwenyekiti wake Komredi Abbas Mtemvu leo Novemba 9, 2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi katika Halmashauri ya Manispaa Kinondoni katika majimbo ya Kinondoni na Kawe.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa akitokea Dar es salaam Juma S. Gaddafi alisema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anahangaika usiku na mchana kuwasaidia watu wanyonge na masikini hivyo ni wajibu wa kamati kupita na kukagua pesa zinazotolewa zinafanyiwa kazi inavyotakiwa na kamati iliridhia maendeleo yake.

Mhe. Gaddafi alisema, "Sisi tumefanya ziara kwenye majimbo hayo na miradi yake, tumeona pesa zinavyokwenda zinaenda vizuri na zinatumika kama zilivyoombwa, niwapongeze Mstahiki Meya na timu yake, wabunge wa Kinondoni na Kawe na wataalamu wote."

Naye mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ambaye ndiye msimamizi mkuu wa miradi hiyo alisema wamejikita kwenye afya, elimu  na barabara, "Sisi jukumu letu ni kusimamia miradi hiyo kwenye viwango, ili kuwe na thamani ya pesa  na pia kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati, mfano miradi ya shule ikamilike kwa wakati na ibebe waanafunanzi kwa wakati na zaidi katika kiwango cha maghorofa kutoka na uhaba wa Ardhi Katika Mkoa huu, alisema. 

Aidha RC Chalamila alieleza ujengaji wa madarasa na vituo vya afya kwa maghorofa  inasaidia kuzuia kusambaa kwa majengo kutoka ardhi ndogo ya mkoa wa DSM kutoka na wingi wa watu wake hivyo aliwapongea sana watendaji wote kwa malengo yaliyokamilishwa hali itakayorahisisha kueleweka zaidi kwa wapiga kura kipindi kijacho cha  uchaguzi 2025.

Miradi iliyokaguliwa kwa jimbo la Kinondoni ni miradi mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 4.325 ambayo ni ujenzi kituo cha afya, madarasa na vyoo shule ya msingi Mapinduzi, uwanja wa mpira na barabara (Mwenge), huku jimbo la Kawe miradi mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 2.799 nayo ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari Changanyikeni, nyumba ya mwalimu shule ya sekondari Godwin Gondwe na ujenzi wa mabweni, madarasa na vyoo Mbweni.

Miradi mingi imekamilika asiliamia 90 na ipo michache ambayo ipo kwenye hatua za mwisho, imechelewa kutokana changamoto mbalimbali ambayo ni asiliamia 10.

Share: