Kamala harris iwapo chama cha democrat kitamteua kuwa rais na kushinda uchaguzi haita kuwa mara yake ya kwanza kushika madaraka hayo

haitakuwa mara yake ya kwanza kushika madaraka ya urais.

Huko nyuma mnamo 2021, wakati Joe Biden alipolazwa kwa upasuaji na kuchomwa sindano ya nusu kaputi ili afanyiwe uchunguzi wa kawaida wa utumbo mpana, Harris alishikilia madaraka kwa dakika 85.

Katika muda wake wa zaidi ya saa moja madarakani, Harris alitekeleza majukumu yake kutoka katika ofisi ya jengo la Magharibi mwa Ikulu ya White House.

Wakati huo, afisa wa habari wa Ikulu ya White House Jen Psaki alisema uhamishaji wa madaraka katika mazingira kama haya haujawahi kutokea, na ni sehemu ya mchakato uliowekwa katika katiba ya Marekani.

Marekebisho hayo ya 25 ya katiba yanasema: "Iwapo rais ataondolewa madarakani au atafariki au kujiuzulu, makamu wa rais atakuwa rais."

Kipindi cha mpito cha mamlaka kieelezewa kwa kina katika sehemu ya tatu ya marekebisho, mabadiliko ya katiba yaliyofanywa kutokana mauaji ya Rais Kennedy mnamo 1963.

Share: