Leo tarehe 4/3/2024 mchana huu nimekabidhi rasmi barua yangu kwa Katibu wa Kamati Maalum ya Uchaguzi Taifa
Halmashauri Kuu ya Chama Taifa iliyokutana kwenye Ukumbi wa Hakainde Hichilema uliopo kwenye Jengo la Maalim Seif (Makao Makuu ya Chama cha ACT Wazalendo) imeridhia uamuzi wa Ndugu Juma Duni Haji kujitoa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa wa ACT Wazalendo.
"..Leo tarehe 4/3/2024 mchana huu nimekabidhi rasmi barua yangu kwa Katibu wa Kamati Maalum ya Uchaguzi Taifa na kuinakilisha barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa Chama na Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uchaguzi Taifa kwa taarifa na hatua zao, kuhusu kujitoa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama Taifa.
"Nimechukua uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 11(3)(7) na Ibara ya 76(1)(p) na Ibara ya 111(3) zikisomwa pamoja, juu ya haki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa Kiongozi, kazi na wajibu wa Halmashauri Kuu ya Chama kuwa ni "kujadili na kuidhinishwa na majina ya wagombea wa nafasi za Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama"-amesema Juma Haji Duni.
Akizungumza kuhusu sababu za kuondoa jina lake, Mwenyekiti wa Chama Ndugu Juma Duni Haji alisema (nanukuu);
"Nimefikia uamuzi huo (wa kujitoa kugombea Uenyekiti wa Chama Taifa) kwa sababu zifuatazo;
1. Kuzingatia maslahi mapana ya Taasisi yetu
2. Kuzingatia ushauri, maoni na au mapendekezo ya Viongozi wenzangu
3. Kuondoa taharuki iliyojitokeza
4. Kuimarisha umoja na maelewano miongoni mwetu
5. Kuelekeza nguvu zote sote dhidi ya washindani wetu wa kisiasa na kutotoa nafasi ya mgawanyiko miongoni mwetu
6. Kumuachia Ndugu Othman Masoud Othman akabidhiwe nafasi hii aendeleze mapambano ya kudai haki
7. Nimetekeleza haki ya kikatiba.."