Jina la tume ya uchaguzi nchini tanzania (nec) litabadilika kuanzia ijumaa aprili 12, 2024

Kulingana na taarifa yake kwa vyombo vya habari, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mobhare Matinyi amesema kuwa chombo hicho kinachoratibu michakato ya uchaguzi nchini Tanzania, sasa litakuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi 'Independent National Electoral Commission', kwa lugha ya kiingereza.

“Tunapenda kuvitaarifu vyombo vyote vya habari kwamba, kufuatia tangazo la Serikali namba 225 la Machi 29, 2024 Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024, itaanza kutumika rasmi Aprili 12, 2024," sehemu ya taarifa hiyo ilisema.

Uamuzi huo unakuja miezi minne baada ya wadau wa vyama vya siasa nchini Tanzania kutaka mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, muundo wa tume hiyo mpya bado haukawekwa wazi.





Share: