Inec: mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji Jacobs Mwambegele amesema wakati wa uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura Mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika Vituo vya Kuandikisha ili kusaidia kuweka uwazi katika zoezi hilo

Amesema “Mawakala watasaidia kutambua wanaojiandikisha, hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima, japo hawaruhusiwi kuwaingilia Watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.”

Tume imetangaza uzinduzi wa Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika Julai 20, 2024 Mkoani Kigoma

Share: