Hospital ya mama samia muheza imeshaanza huduma

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Itikadi,Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda amebainisha kuwa Hospitali ya Mama Samia iliyojengwa Wilayani Muheza tayari inatoa huduma ya afya kwa Watanzania wote na wananchi wa wameheza wameanza kunufaika kwa uwepo wa hospitali hiyo.

Makonda amebainisha hilo mara baada ya kumtaka Mkurugenzi wa Muheza kueleza juu ya hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo Mkurugenzi alimthibitishia mbele umma kuwa tayari imekamilika kwa kiasi kikubwa na huduma zinatolewa.

Pia, mkurugenzi amemueleza Mwenezi Makonda kuwa huduma zote zilizopangwa kutolewa katika hospitali hiyo zimeshaanza kutolewa kwa asilimia 75% ambapo asilimia 25% zilizobaki ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa majengo machache ambayo tayari wameshaombea fedha na ndani ya mwaka huu wa bajeti wameshahaidiwa kupatiwa fedha hizo.

Share: