Haki itendeke kwa mama anayedaiwa shamba la hekari 42

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametoa maelekezo ya CCM inayoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Same kuhakikisha Mwanamama anayedai shamba lake la ukubwa wa hekari 42 apatiwe haki yake pasipo bugza wala janja janja.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wananchi wa Same Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back to Back.

Aidha, Mwenezi Makonda amekemea tabia za baadhi ya watendaji kutengeneza mazingira ya kutaka kupewa rushwa ilikusudi ndio kutenda haki kwa Wananchi.

Share: