Frank habineza na Philippe mpayimana kupambana na Paul kagame nafasi ya urais rwanda.

Kulingana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC), wawili hao, na Rais Paul Kagame ndio wagombea watatu pekee waliofuzu kisheria kuwania nafasi hiyo ya uongozi wa juu kabisa nchini Rwanda.

Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Green Party of Rwanda, Frank Habineza na mgombea binafsi Philippe Mpayimana ambao pia waliwania kiti hicho kwenye uchaguzi wa urais wa Rwanda 2017, ndio wametimiza vigezo vya kisheria vya kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Rwanda mwaka huu.

Habineza alipata asilimia 0.45 ya kura zote huku Mpayimana akivuna asilimia 0.72 ya kura zote katika uchaguzi ambao Kagame aliibuka mshindi.

Rais wa sasa wa Rwanda, Paul Kagame, ambaye amekuwa uongozini tangu 2000, atawania kupitia chama tawala cha Rwanda Patriotic Front (RPF).

Share: