EAC yataja amani, usalama na utulivu kama kivutio kikubwa cha mikutano ya kimataifa Arusha

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bi. Veronica Nduva ameishukuru Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu nchini Tanzania, akisema suala hilo limekuwa Kivutio kikubwa cha mikutano ya Kimataifa kufanyika Mkoani Arusha na maeneo mengineyo

Bi. Nduva ametoa kauli hiyo mapema leo Alhamisi Novemba 21, 2024 kwenye Ukumbi wa mikutano Makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati alipokutana na wanahabari kueleza kuhusu maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayokutanisha Wakuu wa nchi zote za Pembe hiyo ya Afrika.

Akizungumzia ratiba za Maadhimisho hayo ya Miaka 25 ya Jumuiya ya afrika Mashariki yatakayofanyika Kwenye kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC Jijini Arusha, Bi Nduva ameeleza kuwa kutakuwa na Tamasha la Kitamaduni litakalojumuisha Washiriki kutoka nchi zote za EAC,huku Vikao mbalimbali vikijadili kuhusu Amani na Usalama kwa EAC pamoja na Changamoto na mafanikio ya Jumuiya hiyo.


Share: