Viongozi Watatu wa Upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wameitisha maandamano Nchi nzima mnamo Januari 20, 2024 siku ambayo Rais Félix Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa kwa Awamu ya Pili kuwa madarakani.
Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa 73% ya kura, kulingana na Tume ya Uchaguzi, lakini matokeo hayo Wapinzani kadhaa wanadai kuna udanganyifu na wanataka Uchaguzi urudiwe.
Wito huo umetolewa na mmoja wa waliokuwa wagombea Moïse Katumbi ambaye kwa mujibu wa matokeo rasmi alipata 18%, wengine ni Martin Fayulu (5%) na Anzuluni Bembe (1%).
Wamedai kuwa kulikuwa na udanganyifu na ujazo wa kura katika uchaguzi huo.
Share: