Dorothy semu: vijana wa siku hizi wanapenda kubembelezwa

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu anasema “Tuliosoma zamani kidogo tulisoma somo la Siasa, hiyo ilitujenga kuamini Vijana wote ni sehemu ya Siasa na kutambua ukifikisha umri wa Miaka 18 ni jukumu lako kwenda kupiga kura, sio kubembelezwa au kushawishiwa.”

Ameongeza “Mfumo wa sasa ni uhuru wa kuchagua, Vijana wa siku hizi wanapenda kubembelezwa, uhuru umezidi na hawataki kutumia uwezo wao wa kuwa sehemu ya uongozi au mabadiliko, wanatakiwa watambue mabadiliko hayatokei tu bila ushiriki wao.”

Amesema Vijana wengi wanapenda kupata vitu vingi kwa haraka bila kupitia mchakato stahiki, amedai wanakosa muda wa kujifunza mambo na wanataka matokeo ya harakaharaka

Share: