Mara baada ya kuongoza kwa kura za urais, watu mbalimbali waanza kutuma salamu za pongezi kwa Donald Tump
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban wamekuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza duniani kumpongeza Donald Trump - anayetarajiwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais nchini Marekani.
Uchaguzi wa rais mpya sio suala kubwa kwa Marekani pekee kwani kiongozi mpya katika Ikulu ya White House anaweza kubadilisha sera ya mambo ya nje pamoja na kubadili msimamo wake kuelekea Marafiki na maadui zake kimataifa.
Katika taarifa yake, Benjamin Netanyahu alizungumzia "kurejea kwa historia kubwa zaidi", akiongeza kuwa kurejea kwa Trump ofisini kunatoa "mwanzo mpya kwa Marekani kujitolea kwa nguvu kwa muungano mkubwa kati ya Israeli na Marekani".
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ambaye ni shirika wa karibu wa Trump, alisema uchaguzi wa Trump ulikuwa "ushindi unaohitajika sana kwa ulimwengu". "Urejesho mkubwa zaidi katika historia ya kisiasa ya Marekani!" aliandika kwenye mtandao wake wa X.
Bw. Orban alikuwa ameidhinisha waziwazi ombi la Bw. Trump la kutaka kuchaguliwa tena, baada ya kuwa kiongozi wa kwanza na pekee wa Umoja wa Ulaya kumuunga mkono mwaka 2016. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alimpongeza Trump, akisema yuko tayari kufanya kazi pamoja naye kama hapo awali, "kwa heshima na matarajio. Kwa amani na ustawi zaidi".
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alisema: "Ninatarajia kufanya kazi na Trump katika miaka ijayo".