Democratic na republican kuchagua watakao peperusha bendera zao nafasi ya urais

Nchini Marekani leo ni Super tuesday - Usiku muhimu kwa majimbo takribani kumi na sita kupiga kura za mchujo kuamua wagombea urais wa vyama viwili vikubwa nchini Marekani.

Vyama vya Democratic na Republican watakuwa wakichagua watakaopeperusha bendera za vyama vyao kwenye nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Novemba mwaka huu.

Rais Joe Biden anayewania muhula wa pili bila ya upinzani mkubwa kupitia democratic anatazamiwa kupata ushindi wa wazi kwenye majimbo 16 na jingine moja lililo chini ya milki ya Marekani.

Kwa Upande wa Republican Nikki Haley anayo nafasi ya mwisho kusalia kwenye kinya n'ganyiro dhidi ya Donald Trump anayeonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kupeperusha bendera ya Republican.

Share: