Taarifa hizo zina lengo la kusababisha hofu na taharuki
Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi, CP Hamad Khamis amesema taarifa zinazosambazwa na Chama cha ACT Wazalendo katika Mitandao ya Kijamii kuhusu hali ya uhalifu kuongezeka Visiwani Zanzibar ni za upotoshaji na wanaofanya hivyo wana malengo Binafsi ya Kisiasa
Amesema “Taarifa hizo zina lengo la kusababisha hofu na taharuki, pia baadhi ya Viongozi wa ACT-Wazalendo hapa Visiwani wamekuwa wakishawishi Wananchi wasijiunge na Vikundi vya Ulinzi Sirikishi kwa madai hiyo ni Sera ya chama kilicho madarakani.”
Baada ya kutokea kifo cha Katibu wa ACT-Wazalendo (Jimbo la Chaani), Ali Bakari Ali (Machi 29, 2024), chama hicho kilidai Ali alitekwa, alishambuliwa na kutupwa na Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi, pia kikadai kuna vikundi vya kihalifu vinavyojiimarisha kila siku bila Jeshi la Polisi kuonesha uwezo wa kuvidhibiti.