Chama tawala nchini afrika kusini (anc) kinasema kuwa kimepiga hatua katika juhudi za kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kinasema kuwa kimepiga hatua katika juhudi za kuanzisha serikali ya umoja wa kitaifa baada ya kupoteza idadi kubwa ya wafuasi wake katika uchaguzi wa hivi majuzi.

Lakini Katibu Mkuu wa chama hicho Fikile Mbalula alisema chama bado hakiko tayari kutangaza maelezo ya makubaliano hayo.ANC ilipoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 30 katika uchaguzi wa Mei 29, na kupata 40% ya kura.

Hii ina maana ilihitaji kuungwa mkono na vyama vingine ili Rais Cyril Ramaphosa aweze kusalia madarakani. Bunge jipya linakutana kwa mara ya kwanza Ijumaa, wakati linapotarajiwa kumpigia kura rais. Bw Ramaphosa anatarajiwa kuhifadhi kiti chake. "Tunazungumza na vyama vya kisiasa tunapozungumza hivi sasa," Bw Mbalula aliambia wanahabari baada ya mkutano wa maafisa wakuu wa chama hicho, akiongeza kuwa hawezi kutoa maelezo zaidi.

Alisema itakuwa kuhamia kituo cha kisiasa, kwa sababu vyama vilivyojitenga na ANC vilivyo upande wa kushoto vimesema havitajiunga.Alisema vyama vikiwemo vinavyounga mkono biashara vya Democratic Alliance (DA) vimekubaliana kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.Lakini ANC na DA hawajaafikiana kuhusu jinsi gani hasa watashirikiana, Bw Mbalula aliongeza.

"Kama DA ingepata baadhi ya vitu hivi inavyotaka ina maana ANC itakuwa imekufa," alisema.DA ilishika nafasi ya pili katika uchaguzi huo kwa asilimia 22 ya kura.Rais Cyril Ramaphosa hapo awali ameshutumu DA - ambayo inaungwa mkono hasa na watu walio wachache na wa rangi - kwa "uhaini" na "wapinzani".

Mpango wowote na DA hautakuwa maarufu miongoni mwa wanaharakati wengi wa ANC.Chama hicho ni mtetezi wa uchumi wa soko huria, ambapo kinakinzana na mila za mrengo wa kushoto za ANC, na kina sifa ya kuwakilisha maslahi ya wazungu walio wachache.

Share: