Ccm iringa yasisitiza umoja na mshikamano kuelekea uchaguzi

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daud Yassin amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatakiwa kuwa wamoja ili waweze kushinda kwa kishindo.

Yassin amesema kila Kiongozi wa CCM mkoa wa Iringa anatakiwa kutimiza wajibu wao ili kuendelea kuimarisha Umoja na mshikamano walionao sasa hadi uchaguzi uishe kwa ushindi mkubwa wa kishindo. 

“Serikali ya CCM inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Serikali ya wananchi. Kazi yetu ni kuhakikisha changamoto na kero za wananchi tunazitafutia ufumbuzi,” amesema Yassin.

Aidha amewataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Nyalumbu kuhakikisha kuwa wanawachagua wagombea wenye sifa na wanaokubalika kwa wananchi na amekemea mtindo wa kuweka maslahi binafsi badala ya maslahi ya chama. 

“Ikitokea mtu anakubalika na wananchi, tuweke pembeni tofauti zetu na tukipiganie Chama Cha Mapinduzi, chama kwanza sisi baadae,”

Share: