Bil.754/- zatekeleza miradi ya maendeleo kilimanjaro

Hata hivyo, amesema katika Jimbo la Vunjo pekee Sh.Bilioni 3.8 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu amesema kwa kipindi cha miaka miwili ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoa huo umepokea takribani Sh.Bilioni 754 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza katika uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchuguzi ya CCM 2020-2025 ya Jimbo la Vunjo leo, amesema Mhe. Rais ameutendea haki mkoa huo na kati ya fedha hizo Sh.Bilioni 92.29 zimejenga miundombinu ya afya hususan hospitali za Wilaya, Majengo ya huduma za dharura, majengo ya wagonjwa mahututi, nyumba aa watumishi, vifaa tiba hususan ni vile vya majengo ya kufanyia upasuaji wa dharura, mionzi pamoja na ununuzi wa madawa.

 Aidha, amesema Sh. Bilioni 70.3 zimetumika kujenga shule mpya za Sekondari pamoja na msingi, nyumba za walimu pamoja madarasa ya awali. 

Hata hivyo, amesema katika Jimbo la Vunjo pekee Sh.Bilioni 3.8 zimepokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Share: