Bassirou diomaye faye anaonekana kumzidi waziri mkuu wa zamani amadou ba kwenye uchaguzi mkuu senegal

Rais anayemaliza muda wake Macky Sall amewataka kuacha kushangilia mapema kabla matokeo rasmi hayajawekwa wazi.

Mgombea wa Urais nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye anakaribia kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili.

Faye, mwenye miaka 43, anaonekana kumzidi Waziri Mkuu wa zamani, Amadou Ba kulingana na matokeo ya awali yalichopashwa kwenye vyombo vya habari vya ndani na kwenye mitandao ya kijamii.

Vituo vya televisheni na radio nchini humo vilitoa matokeo ya vituo 16,000 vya kupigia kura nchini humo.

Hata hivyo, Rais anayemaliza muda wake Macky Sall amewataka kuacha kushangilia mapema kabla matokeo rasmi hayajawekwa wazi.

Share: