Afrika kusini: jacob zuma amesema chama chake kitaungana na kambi ya upinzani bungeni ili kukwamisha mipango ya serikali

Rais wa zamani na Kiongozi wa Chama kipya cha uMkhonto weSizwe (MK), Jacob Zuma amesema Chama chake kitaungana na Kambi ya Upinzani Bungeni ili kukwamisha mipango ya Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa.

Zuma ameendelea na msimamo kuwa Uchaguzi Mkuu wa Wabunge uliofanyika Mei 29, 2024 ulivurugwa na Serikali na hivyo anataka Matokeo yote yafutwe kwasababu ANC haiwezi kuwa suluhisho la matatizo ya nchi hiyo.

MK chini ya Zuma aliyejiuzulu Urais mwaka 2018 kutokana na kashfa za Rushwa, ambacho kilishinda Viti 58 vya Ubunge, kitaungana na Vyama vya Economic Freedom Fighters kinachoongozwa na Julius Malema na United Democratic Movement.

Share: